Wagalatia 2:20-21
Hujambo na karibu tujifunze neno lamungu pamoja msalaba wa yesu kristo ni lazima ndio mada yetu. Wagalatia 2:20-21. Jina langu ni david ungai wimbo alafu tuendelee
Naam karibu tujifunze pamoja kutoka waraka wa Paulo kwa Wagalatia 2:20-21, msalaba wa yesu ni lazima.
Makanisa mengi karibu yote huonyesha na kuanika yote wazi msalaba maana katika Imani na mafundisho ya ukristo msalaba ni lazima. Warumi walitumia msalba kuwatesa na kuhukumu waasi.
Sisi wakristo huzingatia na kuhimiza ujumbe na somo la msalaba. Somo na ujumbe wa kuteswa kwake bwana wetu yesu kristo msalabani kwa sababu ya makossa na dhambi zetu. Ilikuwa muhimu kristo afe msalabani kwaajili na kwasabau yetu sisi wenye dhambi. Nasoma sasa waraka wa Paulo kwa Wagalatia 2:20-21
Ilitupate kuelewa umuhimu wa ujumbe wa msalaba. Tunazo kweli tatu
1 kusulubiwa kwake yesu kumeandikwa katika vitabu vyote vya injili; mathayo marko, luka na yohana. Hata waleo ukienda Israeli utauona mlima kaivari aliposulubiwa yesu kristo. Pamoja na hayo waandishi wa vitabu wa kirumi waliandika mengi kuhusu kusulubiwa kwake yesu
Jesephus, mwalimu wa historia myahudi pia ameandika mengi kuhusu kuslubiwa kwake yesu pamoja na hayo, pilato ndoye aloyemuhukumu yesu kusulubiwa msalabani
2 uvumbuzi wa msalaba una fundisho la kiroho. Paulo asema nimesulubiwa pamoja na kristo. Yaani kristo aliposulubiwa msalabani pia na Paulo alisulubiwa pia wewe na mimi
Pilato naye alisema sioni makossa ya mru huyu. Hata hivyo aliweka sahihi keisto asulubiwe.
Uvumbuzi huu ni wetu pia. Twaishi lakini sio sisi bali ni kristo aliyesulubiwa, bwana asifiwe. Funzo au somo la kiroho kwa yeyote anayemwamini yesu
3 msalaba ni ukweli ulopo na muhimu kwa ukombozi kwetu kutoka ndambini. Ndiyo njia ya pekee ya kusamehewa dhambi zetu. Mungu baba anapotazama mkristo huuona msalaba wa yesu maana ni katika msalaba dhambi ziliondolewa na kusamehewa kabisa. Kama vile magharibi na mashariki ziko mbali na hazitakutana ndivyo dhambi zetu zimeondolewa kutoka kwetu na hazitarudi temehesabiwa aki katiak kristo
Huo ni ukweli na hauwezi kuondolewa na yeyote. Ujumbe wa msalaba ni wa unyenyekevu kwasabau ya msalaba wa yesu niko tayari kunyenyekea kwake yesu kristo na nina uhakika wa kusamehewa dhambi zangu na kupata utakaso
Kwa hiyo msalaba ni lazima na muhimu kwa maisha yetu ya wokivu