Zaburi 24
Hujambo mpenzi msikilizaji, leo twalichambua fungu la neon la mungu kutoka zaburi 24. Jina langu ni david Mungai. Karibu wimbo alafu tuendelee
Naam karibu tena tujifunze neon la mungu , zaburi 24. Ujumbe huu twautoa zaburi. Zaburi ni kitabu cha nyimbo ziliimbwa kama wimbo hata leo, kunayo madhehebu ambayo huimba zaburi. Zaburi hii itatutia nguvu za kiroho kichwa cha zaburi hii ni mfalme wa utukufu. Bwana wetu na mfalme wetu yesu kristo alipaa kwenda mbinguni akionekana na mtume wake na vivyo hivyo ndivyo atakavyorudi tena Yesu Kristo yuarudi tena bila shaka, kutuchukua ili alipo nasi tuwepo.
Nasoma zaburi 24
1 Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana, Dunia na wote wakaao ndani yake.
2 Maana ameiweka misingi yake juu ya bahari, Na juu ya mito ya maji aliithibitisha.
3 Ni nani atakayepanda katika mlima wa Bwana? Ni nani atakayesimama katika patakatifu pake?
4 Mtu aliye na mikono safi na moyo mweupe, Asiyeiinua nafsi yake kwa ubatili, Wala hakuapa kwa hila.
5 Atapokea baraka kwa Bwana, Na haki kwa Mungu wa wokovu wake.
6 Hiki ndicho kizazi cha wamtafutao, Wakutafutao uso wako, Ee Mungu wa Yakobo.
7 Inueni vichwa vyenu, enyi malango, Inukeni, enyi malango ya milele, Mfalme wa utukufu apate kuingia.
8 Ni nani Mfalme wa utukufu? Bwana mwenye nguvu, hodari, Bwana hodari wa vita.
9 Inueni vichwa vyenu, enyi malango, Naam, viinueni, enyi malango ya milele, Mfalme wa utukufu apate kuingia.
10 Ni nani huyu Mfalme wa utukufu? Bwana wa majeshi, Yeye ndiye Mfalme wa utukufu.
Katika fingu hili la neon la mungu, twaon bwana wetu yesu kristo kuwa muumbaji, mkombozi, na mshindi wa ajabu
Kuanzia mstari wa kwanza na mstari wa pili, bwana wetu yesu kristo ni muumbaji kama anavyoelezawa katika kitabu cha mwanzo sura ya kwanza kwa neno tu akaumba mimea samaki ndege wa angani na vitu vyote hata wahudumu.
Pamoja na haya zaburi hii yamwonyesha bwana yesu kristo kuwa ndiye mkombozi aliye makatifu.
Yesu kristo ahitimu kuwa huwakomboa wenye dhambi kutoka kwa mauti ya milele.
Pamoja na hayo twajua na kuamini ya kwamba kama mfalme atarudi tena kwa kishindo kikuu na kuanzisha utawala wake wa maelfu
Yesu kristo ndiye mfalme wa wafalme na ndiye bwana na mkombozi wetu.