II Wakorintho 11:16-33
Hujambo msikilizaji wangu mpenzi na karibu tujifunze neno pomoja. Jina langu ni david Mungai. Leo twalichambua neno la Mungu kutoka kitabu cha 2 Wakorintho 11:16-33, MATESO YAKE PAULO
Wimbo halafu tuendelee.
Naam, karibu tena tujifunze neno pamoja. NASOMA
16 nasema tena mtu asidhani ya kuwa mimi ni mpumbavu lakini mjaponidhania hivi mnikubali kama mpumbavu ili mimi name nipate kujisifu ngaa kidogo
17 ninenalo silineni agizo la bwana bali kama kwa upumbavu katika ujasiri huu wa kujisifu
18 kwa sababu wengi wanajisifu kwa jinsi ya mwili mimi name najisifu
19 ninyi kwa kuwa mna akili mnachukuliana na wajinga kwa furaha
20 maana mwachukuliana na mtu akiwatia utumwani akiwameza, akiwateka nijara akijikuza akiwapiga usoni
21 nanena kwa jinsi ya kujidhili kana kwamba sisis tulikuwa dhaifu . walakini akiwa mtu anao ujasiri kwa lolote nanena kipuuzi foolishness mimi name ninao ujasiri
22 wao ni waebrania . na mimi pia wao ni waisraeli. Na mimi pia wao ni uzao wa ibrahimu .na mimi pia
23 wao ni wahudumu wa kristo nenea kiwazimu mimi ni Zaidi katika taabu kuzidi sana katika vifungo kuzidi sana katika mapigo kupita kiasi katika mauti mara nyingi
24 kwa wayahudi mara tano nalipata mapigo arobaini kasoro moja
25 mara tau nalipigwa na bakora mara moja nalipigwa kwa mawe mara tatu nalivunjikiwa jahazi kuchwa kucha nimepata kukaa kulindini
26 katika kusafiri mara nyinyi hatari za mito hatari za wanyonganyi hatari kwa mataifa mengine hatari za mjini , hatari za jangawani hatari za baharini hatri kwa ndugu za uongo
27 katika taabu na masumbufu katika njaa na kiu katika kufunga mara nyingi katika baridi na kuwa uchi
28 baghariri (apart from such) ya mambo ya nje yako yanijiayo kila siku ndiyo maangalizi ya makanisa yote
29 ni nai aliye dhaifu nisiwe dhaifu name ? ni nai asiyekwazwa name nisichukiwe?
30 ikinibidi kujisifu nitajifia mambo ya udhaifu wangu
31 Mungu, baba wa bwana Yesu aliye mtukufu hata milele anajua ya kuwa sisemi uongo
32 Huko Dameski liwali wa mfalme arefa alikuwa akiulinda mji wa wadameski ili kunikamata
33 nami nikatetemshwa ndani ya kikapu katika dirisha la ukutani nikaokoka katika mkono wake.
kusema kweli, Paulo aliyapitia mazito, kwa ajili ya injili baadhi ya wakristo wakorintho walimwelekea mambo ya uongo
Katika mstari wa 16-18 paulo atuonye kwamba mpumbavu hujikuza yeye mwenyewe binafsi siyo katika bwana na kuhukumiwa Paulo alijivunia kidogo kwa sababu alikuwa mwanadamu tulivyo na kama walivyokuwa wakorintho. Licha ya kuwa tumeokolewa bado twajivunia kwa sababu sisi ni wanadamu lakini kwa neema yake Mungu hutuhurumia waalimu wa uongo, baadhi walijivunia kuwa walikuwa webrania na wajivuna sana mbele ya wakristo waliokuwa wa mataifa mengine. Wazi kabisa waebrania waliwadhihaki wakristo wa mataifa kwa hiyo Paulo awaambia ya kwamba asema kama mpumbavu au mtu asiye na akili timamu kwa ajili ya injili ya Yesu, Paulo aliteswa.
Mst 24 waonyesha ya kwamba Paulo alipigwa mijeledi mara 39 hawangezidisha hapo, kulinganaa na sharia kama tunavyosoma katika kumbukumbu la torati 25:1-3
Pakiwa na mashindanp kati ya watu wakaenda maamuzini n ahao waamuzi wakawaamua na wampee haki mwenye haki ns wamhukumie makossa yule mwovu
2 na iwe ikimpasa kupigwa yule mwovu alazwe chini ya mwamuzi na kupigwa mbele ya uso wake kwa kadiri ya ouvu wake kwa kuhesabu
Aweza kumpiga fimbo arobaini asizidishe asije akaonekana nduguyo kuwa amedharauliwa kwako azidishapo kwa kumpiga fimbo nyinyi juu ya hizi
Pamoja na hayo walimpiga Paulo kwa fimbo hii ilikuwa amri ya watu wa mataifa kwa yeyote aliyesababisha ghasia kam tunavyosoma katika kitabu cha matendo ya mitume 16:22-23
Walimpiga Paulo kwa bakora .mara tatu meli ilimharibika Paulo na mara ya nne katika matendo ya mitume 27 baada ya Paulo kuandika waraka huu wa 2 wakorintho. Pamoja na hayo Paulo aliteseka moyoni. Pamoja na hayo Paulo alisaidiwa kutoroka kwa kutelemshwa na kikapu kwa sababu ya unyonge wake
Hata hivyo maneno ya mstari wa 30 yanipa nguvu katika Imani yangu. 2 wakorintho 11:30 paulo asema ikinibidi kujisifu nitajisifia mambo ya udhaifu wangu
Sis wakristo tu wadhaifu wetu, Mungu katika Kristo bwana hutupatia ushindi usikose kupiga magoti na kumwomba Mungu wetu katika Kristo atupiga nie vita maana sisi ni wa dhaifu lakini Yesu daima ni mshindi.