II Wakorintho 8:7-15
Hujambo na karibu msikilizaji katika matumaini. Leo twalichambua fungu la neno kutoka 2 Wakorintho 8:7-15, kusudi la matoleo yetu.
Jina langu ni David mungai, wimbo halafu tuendelee.
Naam karibu tena tujifunze neno 2 Wakorintho 8:7-15, kusudi la matoleo yetu
Nasoma fungu hili
Lakini kama mlivyo na wingi wa mambo yote, Imani na usemi na elimu na bidii yoye ya na upendo wenu kwetu sisi basi vivyo hivyo mpate wingi wa neema hii pia.
8 sineni ili kuwaamuru bali kwa bidi ya watu wengine nijaribu unyofu wa upendo wenu
9 maana mmejua neema bwana wetu yesu kristo jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu ingawa alikuwa Tajiri ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake
10 Nami katika neno hili natoa shauri langu maana neno hili natoa hili lawafaa ninyi mliotangulia yapata mwaka licha ya kutenda hata kutaka pia
11 lakini sasa timizeni kule kutenda nako ili kama vile mlivyokuwa tayari kutoka vivyo hivyo mkawe tayari na kutimiza kwa kadiri ya mlivyo navyo
12 maana kama nia ipo hukubaliwa kwa kadiri ya alivyo navyo mtu si kwa kadiri ya asivyo navyo
13 maana sisemi hayo ili wengine wapate raha nanyi mpate dhiki
14 bali mambo yawe sawasawa wakati huu wa sasa wingi wenu uwafae upungufu wao ili na wingi wao uwafae ninyi mtakapopungukiwa ili mambo yawe sawasawa
15 kama ilivyoandikwa aliyekusanya vingi hakuzidi wala yeye aliyekusanya vichache hakupungukiwa
Kutoka kwa fungu hili la neno twajifunza kweli nyingi mno au makusudi ya utoaji wa mali yetu kanisani
Ukweli ni kwamba tunapotoa tena kwa upendo twadumisha na kuimarisha Imani yetu katika kanisa la Mungu.
Twapaswa kuonyesha ya kwamba Mungu ametuneemesha kwa neema nyinyi tena mbalimbali neno lasema mst 7 lakini kama mlivyo na wingi wa mambo yote Imani na usemi na elimu na bidii yote na upendo wenu kwetu sisi basi vivyo hivyo mpate wingi wa neema hii pia
Kutoa kwa mioyo mikunjufu twaonyesha utukufu wake mwenyezi Mungu.
Ukweli wa pili ni kuonyesha ukweli wa Mungu kama tunavyosoma katika mstari wa nawe nasoma
8 sineni hii kuwaamuru bali kwa bidi ya watu wengine nijaribu unyofu wa upendo
3 ukweli wa tatu ni kwamba katika utoaji wetu makanisani twamuiga bwana wetu Yesu Kristo ukarimu wa Mungu hauna kifani. Mungu kwa ukarimu wake alimtoa Yesu Kristo kusudi aje hapa duniani afe msalabani kwa niaba na kwa ajili yetu. Maneno ya mstari wa 9 nasoma
9 maana mmejua neema ya bwana wetu yesu kristo jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu ingawa alikuwa Tajiri ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake
Upendo amabao hauna kifani
Ukweli wan ne. na ni muhimu kabisa twatoa kwa sababu twataka kuwasaidia wale hawawezi na ndio wengi duniani Mungu ametuweka nai tuwe mifereji ya baraka kwa watu wengine. Tuwe vichwa siyo mikia kusiwe mtu mhitaji kupindukia kati yetu mstari w 14
Bali mambo yawe sawasawa wakati huu wa sasa wingi wenu uwatoe upungufu wao, ili na wingi wao uwafae ninyi mtakapopungukiwa ili mambo yawe sawa sawa
15 kama ilivyoandikwa aliyekusanya vingi hakuzidi wala yeye aliyekusanya vichache hakupungukiwa
Na hivyo ndivyo tunavyopaswa kufanya katika kanisa lake Kristo maana ndivyo lilivyokuwa kanisa la kwanza
Nasoma kutoka kitabu cha matendo ya mitume 4:32
Na jamii ya watu walioamini walikuwa na moyo mmoja na roho moja wala hapana mmoja aliyesema ya kuwa kitu chote alicho nacho ni mali yake mwnyewe bali walikuwa na vitu vyote shirika
Na hio ndio ukweli wa neno la mungu na ndiyo mapenzi yake.