Kanuni Za Utoaji

October 21, 2018/
Heralds of Hope
Heralds of Hope
Kanuni Za Utoaji
Loading
/
II Wakorintho 8:1-6

Hujambo na karibu tujifunze neno pamoja. Leo twalichambua neno kutoka 2 Wakorintho 8: 1-6, kusudi la utoaji vipawa

Jina langu ni David Mungai. Karibu wimbo, halafu tuendelee.

Naam, karibu tena tujifunze neno. Nasoma kutoka 2 Wakorintho 8:1-6

1 Tena ndugu zetu twawaarifu habari ya neema ya Mungu walioyopewa makanisa ya Makedonia,

2 maana walipokuwa wakijaribiwa kwa dhiki nyingi wingi wa furaha yao na umaskini wao ulikuwa mwingi uliowaongezea utajiri wa ukarimu

3 maana nawashuhudia kwamba kwa uwezo wao na Zaidi ya uwezo wao kwa hiari yao wenyewe walitoa vitu vyao

4 wakituomba sana pamoja na kutusihi kwa habari ya neema hii na shirika hili la kuwahudumia watakatifu

5 tena walitenda hivi si kama tulivyowatumaini tu, bali kwanza walitoa nafsi zao kwa bwana na kwetu pia kwa mapenzi ya Mungu

6 hata tukamwomba Tito kuwatilimizia neema hii kwenu kama vile yeye alivyotangulia kuianzisha

Kanuni za utoaji sadaka na hata msaada kwa ndugu. Jambo la kwanza lapatikana katika maneno ya mstari wa kwanza

Twatoa kwa neema yake Mungu. Kile tulicho nacho ni kwa neema yake Mungu. Ni Mungu hutuwezesha kutoa tena kwa ukarimu

Siyo kwamba tu wema kuliko watu wengine, bali ni kwa neema yake Mungu bila uwezo na nguvu za mwenyezi Mungu ni muhimu kutoa kwa shukrani na roho.

Funzo la pili ni kwamba unaweza kutoa hata ukiwa huna nyinyi, nasoma maneno ya mstari wa 2

Maana waliopokuwa wakijaribiwa kwa dhiki nyingi, wingi wa furaha yao na umaskini wao uliokuwa mwingi uliwaongezea utajiri wa ukarimu wao

Walitoa kwa roho mtakatifu tena ya ukarimu hata wakiwa katika hali za uhitaji mwingi. Haijalishi uhaba au wingi kilicho muhimu machoni mwa Mungu ni kutoa kwa moyo mkunjufu na safi tena kwa ukarimu usisukumiwe kutoa mtu atoe kwa moyo mkunjufu

3 funzo la tatu. Utoaji wetu tutoe kwa ushirika. Ushirika wako na Mungu uwa msukumo unaokusukma kumtolea na kuwatolea wengine kwa upendo wa kumpenda Mungu na kumpenda mkristo mwenzako.

Utoaji huu uwe wa kujitolea. Tusome mstari wa 4-5

Wakituomba sana pamoja na kutusihi kwa habari ya neema hii na shirika hili kwa kuwahudumia watakatifu

Tena walitenda hivi si kama tulivyotumaini tu bali kwanza walijitoa nafsi zao kwa bwana na kwetu pia kwa mapenzi ya Mungu.

Lilikuwa la kumoendeza Mungu na kumtia Paulo motisha wa kuendeleza huduma ya kuhubiri injili na kujitoa kwa Mungu kwake mwili. Huu ni ukweli amabao umejaa katika biblia katika injili ya matt 22:37

Mpende bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote na kwa akili yako yote

Heri kujitoa kwake Mungu mwili, moyo na roho zetu kuwa watumishi na mawakili wake duniani hii. Sisi ni mifereji yake Mungu ya kuwafikishia na wote, habari njema za wokovu

Kusema kweli wachungaji wengi hawajimudu kimaisha maana tumekuwa wachoyo katika utoaji wetu
Na tumwombe kwa unyeyekevu aturejeshee upendo wa kutoa kwa neema na upendo wake Mungu. Ni nini ulicho nacho ambacho hukupewa kwa neema yake Mungu? Zaidi sana Mungu amekuumba kwa njia ya kutisha na kuogofya huwezi kumzidi Mungu katika utoaji ndiyo sababu twatoa kwa shukrani

Bible Distribution

Heralds of Hope partners with in-culture believers to distribute Bibles. By collaborating closely with these partners around the world, we empower them to share God’s Word with their own communities.

Audio Content

Heralds of Hope offers two distinctive teaching programs: The Voice of Hope and Hope for Today, each centered on expository Bible teaching. The Voice of Hope is a weekly, thirty-minute program in English, while Hope for Today is a fifteen-minute international program offered in 26 languages. Both are available through radio and social media platforms.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!